Karibu mtaawasaba, mtaa wa uchambuzi wa mambo yote yahusuyo teknolojia, habari mbali mbali za kiteknolojia. Leo nimekuletea uzi huu uweze kujua kuhusu Wireless Charging, Ni nini Wireless Charging, na ni Simu na vifaa gani zinaweza kutumia Wireless Charger.
1. Wireless Charger ni nini?
Wireless Charging (Chaji cha wireless) ni teknolojia ambayo inaruhusu kupakia umeme umbali mfupi bila nyaya. Pia inaojulikana kama Inductive charging au cordless charging teknolojia hii hutumia magnetiki ya umeme kuhamisha nishati kati ya vitu viwili kupitia koili zilizoundwa kupitisha umeme. Hii hufanyika baina ya kifaa kimoja kinachotoa nishati hiyo na kifaa kingine kinachopokea kwa nia ya kuchaji betri.
Historia ya Wireless Charging
Wireless charging sio kipya sana kukisikia au hata kukiona, Sasa wireless charging ya kwanza iligundulika miaka ya 1864 na James C Maxwell na miaka ya 1888 Heinrich Hertz ndio aliweza kukamilisha project hiyo na kuweza kuonesha dunia kwamba umeme unaweza kupita kwa njia ya wireless. Japo tangu hapo kuna maboresho mengi yalifanika, siwezi kuyaeleza yote hapa cha zaidi ni kukupa faida zaidi ya hii wireless charging ndugu msomaji.
Teknolojia ya Wireless Charging
Kuna viwango mbalimbali vya chager za wireless. Inayojulikana zaidi ni Qi (inayotamkwa kama ‘chee’ neno la kichina), ambayo imetumiwa na makampuni mengi makubwa kama Apple kwenye simu zake za karibuni alizotoa za iPhone, na Samsung pia imekua ikitumia hiyo kwa miaka zaidi ya mitano sasa; Wamefanya pia aina nyingi za coil za wireless za Samsung ambazo hufanya kazi na Qi.
Faida za Wireless Charger
Unajisikiaje unarudi kutoka kazini simu yako ina 8% na mtoto wako wako kaikata ile usb cable unayotumia kuchajia? Of coz usiku huo utahitaji kuomba waya wa jirani na kama anautumia je? utahiaji usubiri kesho uende kariakoo kununua waya mwignine. Au unapaje usumbufu wa kuchomeka simu mara haiingizi au umepita katikati ya waya ukaivuta simu na kuiangusha? Basi mpaka hapo umeshawaza faida walahu moja za wireless charging. Hizi ni baadhi tu ya faida ya wireless charging.
- Inasave muda wako ambao utaweza kuendelea kufanya mambo mengine
- Huchaji simu kwa wakati mfupi wakati mwingine unaweza kuwa umeweka simu kwenye charg kumbe haingizi lakini huwez pata usumbufu huo kwa wireless charging
Simu zinazokubali Charger ya Wireless
Ikiwa simu yako itaonekana katika orodha hii basi kimbia haraka kariakoo kanunue wireless charging.
Apple iPhone: 8, 8 Plus, X
Samsung Galaxy: S9, S9 +, Note 8, S8, S8 +, S7, S7 Edge,Note 5, Note 7, S6, S6 Edge
LG: V30, G6 (toleo la Marekani tu), G4 , G3
Microsoft Lumia: 1520, 1020, 930, 929, 928, 920
Google: Nexus 4, 5, 6, 7, Pixel na Pixel XL 1 na 2
BlackBerry: Priv
Pamoja na kwamba nimeandika matoleo hayo, unaweza kujua kwamba simu yako ina wireless charging kwa kusoma manual inayokuja na box la simu
Unahitaji kuendelea kuwa na Adapter ya waya?
Of coz ndio, bado utahitaji kuwa na adapter ya waya kwa ajili ya kuunganisha Qi kutoka kwenye wall socket kwenda kwenye wireless charger kwani9 Qi si pekee tu kwamba inaweza kupitisha mawimbi ya umeme wireless bado itahitaji suppport ya umeme kutoka kwenye wall socket.
Natumai mpaka sasa nimekupa ushawishi wa kununua wireless charging, Endelea kuwa nami katika makala mbali mbali na pia usisahau kusubscribe kwenye chanell yetu ya YouTube upate maujana ya teknolojia kila siku.
Ambacho sipendi kuhusu wireless charging ni jina lenyewe maana waya bado upo
Je kwa watuiaji Wa Sony Xperia hatuhusiki?