Sasa watumiaji wa Android na iOS wanaweza kujitumia ujumbe kupitia WhatsApp

Kipengele kipya cha "Message Yourself", kitawezesha watumiaji wa simu janja za Android na iOS kujitumia wenyewe ujumbe wa maelezo, picha na zaidi

Alice Maoni 2.5k

Sasa unaweza kujitumia ujumbe kupitia WhatsApp kwani programu hii imeachia kipengele kipya chenye jina  ‘Message Yourself’ kitakachokuwezesha kujitumia Ujumbe Mwenyewe kwa watumiaji kwenye iOS na Android. Kipengele hicho awali kilikuwa sehemu ya jaribio la beta ambalo sasa linapatikana kwa kila mtu.

Sasa unaweza kujitumia ujumbe kupitia WhatsApp kwa Urahisi

Kama ilivyoripotiwa na TechCrunch, programu hii ya kutuma ujumbe inayomilikiwa na Meta lilitangaza kuachia kipengele hicho cha ‘Message Yourself’ jana, na sasa iko njiani kuelekea matoleo ya Android na iOS ya programu. Kwa kipengele hicho, watumiaji wanaweza kujitumia maelezo, vikumbusho, orodha za ununuzi na zaidi.

Kipengele hiki kimekuwa kikipatikana kwenye majukwaa mengine, hasa Telegram, ambayo imekuwa nayo tangu kuzinduliwa, pia programu ya Signal ina kipengele kinachofanana kinachoitwa ‘Note to Self’ kwa muda sasa. WhatsApp ilianza tu kufanyia majaribio kipengele hiki hadharani mnamo Oktoba 2022.  Na kabla ya kipengele hiki kuachiwa, njia pekee ya kujitumia ujumbe  mwenyewe kwa kutumia anwani ‘wa.me/91.’

Jinsi ya kujitumia ujumbe kupitia WhatsApp ‘Message Yourself’

Ili kuanza kutumia kipengele hiki cha kujitumia Ujumbe , ni lazima uwe na toleo jipya la programu ya WhatsApp kwenye simu yako ya Android au iOS. Kama hujasasisha, nenda kwenye Duka la Programu la Google Play/Apple na usakinishe toleo jipya zaidi la programu. Mara baada ya kumaliza, fuata maelekezo haya;

  1. Fungua WhatsApp kwenye simu janja yako
  2. Gonga kitufe cha New Chat – kinapatikana kwenye kona ya juu kulia kwenye iPhone na chini kwenye simu za Android
  3. Hapa, utapata kadi ya mawasiliano na namba yako ya simu kama ‘Message Yourself’ na utaanza kujitumia ujumbe.

Ikiwa bado hujapata kipengele kipya, usijali kwani WhatsApp ilifafanua kuwa inaweza kuchukua wiki kadhaa kwa kusambazwa kwa watumiaji wote. Ningependa kusikia kutoka kwenu mnafikiria nini kuhusu ‘Message Yourself’ kutoka WhatsApp? Shiriki mawazo yako nasi katika maoni hapa chini na endelea kuwa nasi Mtaawasaba kwa habari zaidi za teknolojia kama hii.

CHANZO: TechCrunch
Mwandishi Alice Mhariri Mkuu
Mitandao ya Kijamii
Alice ni mwandishi na mhariri wa makala mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu mwaka 2016. Akiwa hayupo kazini hupendelea kusoma vitabu, kuogelea na kusikiliza muziki
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive