Ni mbunifu wa app ya habari iitwayo âSummlyâ, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 amejikuta amekuwa milionea baada ya Yahoo kuinunua application yake.
Japo haijulikani ni kiasi gani hasa alicholipwa lakini ni mamalioni ya dola.App hiyo itaanza kutumika kwenye products za Yahoo. Summly huchukua habari za mtandaoni na kuzifupisha kuwa na maneno 400 ambazo ni rahisi kusomwa kwenye simu za mkononi.
Pia, mtoto huyo atakuwa mwajiriwa wa Yahoo mwenye umri mdogo zaidi.Nick aliitengeneza app hiyo akiwa na umri wa miaka 25 na kupata uwekezaji kutoka kwa kampuni ya bilionea wa Hong Kong, Li Ka Shing iitwayo Horizons Ventures na kupata shavu kutoka kwa mastaa kama Stephen Fry, Yoko Ono na Ashton Kutcher waliowekeza kwa zaidi ya paundi milioni moja.
App hiyo kwaajili ya simu za iPhone ilianzishwa December 2012 na Summly ilifanya kazi na mitandao zaidi ya 250 duniani.
mhhhh! naona uhai wa yahoo unarudirudi! hivi ule mpango wa microsoft kuinunua yahoo uliishia wapi?