Kuelekea maonesho ya vifaa vya teknolojia ambayo hufanyika nchini Marekani. Kampuni ya Korea kusini ya LG ambayo ni mashuhuri kwa vifaa vya kielektroniki imeonesha TV yenye ukubwa wa inchi 88 na kioo cha OLED chenye uwezo wa kuonesha mpaka 8K.
TV ambayo ni kubwa kabisa kwa sasa pia imetengenezwa na LG na ina ukubwa wa inchi 77 yenye kioo cha OLED na uwezo wa 4K.
Kampuni pinzani ambayo nayo ni ya Korea kusini ya Samsung yenyewe imejikita kwenye kutengeza TV kwa teknolojia ya QLED ambapo unaweza kupata TV yenye ukubwa wa inchi 88 ambayo ni 4K kwa gharama nafuu zaidi.
Kwa sasa runinga zenye uwezo wa kuonesha picha yenye ukubwa 4k zinazidi kuwa maarufu duniani kote na gharama zake zinazidi kuwa nafuu.
Endelea kuwa nasi tuijiandaa kukumulikia mambo mbalimbali yatakayotokea kwenye maonesho ya CES yatakayoanza juma lijalo.