Kampuni ya Sony imezindua simu tatu Xperia XA2, XA2 Ultra and L2 ambazo ni mid-range kwenye maonesho yanayoendelea huko Las Vegas.
Simu hizo zenye kamera zenye uwezo wa kupiga selfie za nyuzi 120 zenye ukubwa megapixeli 8, wakati XA2 Ultra ina uwezo wa kupiga selfie zenye megapixeli 16 bila wide angle.
fingerprint sensor
Hatimaye Sony wameweka fingerprint sensa kwenye simu za Xperia. Simu hizi tatu zitakuwa na fingerprint sensa zitakazoweza kufungua simu pale itakapoguswa. Hata hivyo inasemekana ni matoleo yatakayouzwa Marekani pekee ndio wataweza kutumia fingerprint sensa na nchi zilizobaki duniani fingerprint sensa itakuwa imezimwa.
Kwa haraka haraka hebu tuone sifa za simu hizi tatu
Sifa za SONY XPERIA XA 2 ULTRA, XA 2, L2
Sony Xperia X2 Ultra | Sony Xperia X2 | Sony Xperia L2 | |
Ukubwa wa kioo | 6-inch; 1,920×1,080 pixels | 5.2-inch; 1,920×1,080 pixels | 5.5-inch; 1,280×720 pixels |
Pixeli | 367ppi | 424ppi | 267ppi |
Vipimo (inchi) | 6.4×3.1×0.37 in | 5.6×2.8×0.38 in | 5.9×3.1×0.39 in |
Vipimo (Millimita) | 163x80x9.5 mm | 142x70x 9.7 mm | 150x78x9.8 mm |
Uzito ( Grams) | 210g | 171g | 178g |
Mfumo endeshi | Android 8.0 Oreo | Android 8.0 Oreo | Android 7.1.1 Nougat |
Kamera | 23-megapixel | 23-megapixel | 13-megapixel |
Kamera ya mbele | 16-megapixel (with 8-megapixel 120-degree option) | 8-megapixel with 120-degree lens | 8-megapixel with 120-degree lens |
Video | 4K | 4K | 4K |
Prosesa | Qualcomm Snapdragon 630 | Qualcomm Snapdragon 630 | 1.5GHz quad-core |
Ujazo | 32GB; 64GB | 32GB | 32GB |
RAM | 4GB | 3GB | 3GB |
ujazo wa nje | 256GB | 256GB | 256GB |
Betri | 3,580mAh | 3,300mAh | 3,300mAh |
Fingerprint sensa | Nyuma | Nyuma | Nyuma |
Viunganishi | USB-C | USB-C | USB-C |
Headphone jack | ipo | ipo | ipo |
Sifa maalum | 120-degree sefie photos | 120-degree sefie photos | 120-degree sefie photos |
Bei | TBA | TBA | TBA |