LG kuzindua matoleo mapya ya K8 na K10 kwenye kongamano la MWC 2018

Alexander Nkwabi Maoni 156

Kampuni ya simu ya LG Electronics kutoka Korea kusini imetangaza leo kupitia blogu ya LG Newsroom itazindua matoleo mapya ya simu mbili ambazo ni LG K8 na LG K10 katika kongamano la Mobile World Congress (MWC) inalotarajiwa kuanza jumapili hii inayokuja ya tarehe 25. Simu zote mbili zitaanza kupatikana kwenye maeneo ya Ulaya, Asia, Latin America na Mashariki ya kati.

Simu hizi gharama nafuu ni ingizo jipya katika familia ya simu za bajeti ya K series. Zitakuja na rangi kuu tatu yani nyeusi , bluu na rangi ya dhahabu. Kimuonekano zitakuwa na muonekano wa kung’aa kama zile za matoleo ya mwanzo.

Toleo la K8 2018 linakuja na kamera iliyoboreshwa kuliko mtangulizi wake aliyetoka mwaka jana. LG wanadai kamera za simu hizi zitakuwa na kamera yenye kutoa picha nzuri kwenye mwanga hafifu ukilinganisha na mtangulizi wake.

Wakati K10 inakuja na mtiririko wa simu tatu ambazo ni K10+, K10 na K10 Alpha, wakati K8 haitakuwa na mfuatano, itakuwa na simu moja tu ya K8. Kwa sasa hakuna taarifa zozote kuhusu bei na lini zitaanza kupatikana, hata hivyo kampuni ya LG wamethibitisha simu hizi zitakuwa kwenye kundi la simu za bajeti ndogo.

tukiachana na simu hizi mbili za bajeti ndogo, tetesi zinadai LG wanatarajia kuzindua toleo jipya lililoboreshwa zaidi la simu yake V30 ambayo inasifika kwa sifa kemkem za kamera nzuri na software inayotumia Artificial Intelligence.

Hizi ni baadhi ya sifa ya simu hizi mbili za bajeti zinazotarajiwa kuzinduliwa siku chache zizajo kwenye onesho kubwa kabisa kwenye dunia ya teknolojia.

Sifa za K10:

  • Chipset: 1.5 GHz Octa-Core
  • Kioo: 5.3-inch HD In-cell Touch (1280 x 720 / 277ppi)
  • RAM:
    • K10+ : 3GB RAM / 32GB ROM / microSD (inayoweza kuongezwa mpaka 2TB)
    • K10: 2GB RAM / 16GB ROM / microSD (inayoweza kuongezwa mpaka 2TB)
    • K10α : 2GB RAM / 16GB ROM / microSD (inayoweza kuongezwa mpaka 2TB)
  • Kamera:
    • K10+ : Nyuma 13MP / Mbele 8MP or 5MP (Wide)
    • K10: Nyuma 13MP / Mbele 8MP or 5MP (Wide)
    • K10α : Nyuma 8MP / Mbele 5MP
  • Betri: 3,000mAh (inatoka)
  • Mfumo endeshi: Android 7.1.2 Nougat
  • Ukubwa: 148.7 x 75.3 x 8.68mm
  • Uzito: 162g
  • Mtandao: LTE / 3G / 2G
  • Muunganisho: Wi-Fi (802.11 b, g, n) / Bluetooth 4.2 / USB 2.0 Type B / NFC
  • Rangi:
    • K10+: Moroccan Blue / Terra Gold
    • K10 : Aurora Black / Moroccan Blue / Terra Gold
    • K10α: Aurora Black / Terra Gold
  • Sifa zingine: Fingerprint Scanner / FM Radio / Flash Jump Shot / Music Flash /

Sifa za K8:

  • Prosesa: 1.3 GHz Quad-Core
  • Kioo: 5.0-inch HD On-cell Touch (1280 x 720 / 294ppi)
  • RAM: 2GB RAM / 16GB ROM / microSD (inayoweza kuongezwa mpaka 32GB)
  • Kamera: Nyuma 8MP / Mbele 5MP
  • Betri: 2,500mAh (inatoka)
  • Mfumo endeshi: Android 7.1.2 Nougat
  • Ukubwa: 146.3 x 73.2 x 8.2mm
  • Uzito: 152g
  • Mtandao: LTE / 3G / 2G
  • Muunganisho: Wi-Fi (802.11 b, g, n) / Bluetooth 4.2 / USB 2.0 Type B
  • Rangi: Aurora Black / Moroccan Blue / Terra Gold
  • Sifa zingine: FM Radio / Flash Jump Shot / Music Flash / Time Helper / Quick Capture / Quick Shutter
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive