Utangulizi: Spark 8
Kampuni ya simu ya Tecno leo imezindua simu ya gharama nafuu ya Spark 8 ambayo ni muendelezo wa toleo lililopita la Spark 7 ambayo ilitoka mapema mwanzoni mwa mwaka 2021. Simu ndio simu ya kwanza kuachiliwa ikiwa na nembo ya “Stop at Nothing” iliyoanza kutumika hivi karibuni.
Simu hii inaungana na simu zingine kutoka familia ya TECNO ikiwemo Phantom X, Camon 17 Pro na Spark 7P ambazo tayari ziko sokoni.
Kampuni hii ya China inazidi kuteka soko la simu kwa nchi za kiafrika hasa kwa kujikita kwenye kuachia simu za gharama nafuu. Kampuni hii yenye mtindo wa kuachia simu hizi bila kuzitangaza, hivyo basi usishangae kukutana na simu hii madukani bila kuwa na matangazo yoyote.
Muonekano wa Spark 8
kimuonekano, simu ya Spark 8 inakuja na kioo cha IPS LCD chenye upana wa inchi 6.5 na uwezo wa kuonesha picha za HD+ zenye mpaka ukubwa wa 1600 X 720. Juu ya kioo kuna kamera ya selfie yenye umbo la chozi (tear drop) na upande wa nyuma ina kamera kubwa mbili na flashi, pia kuna sensa ya fingerprint.
Kamera za Spark 8
inakuja na kamera kubwa yenye uwezo wa kupiga picha zenye ukubwa wa 16 MP na kamera ndogo yenye kupiga picha zenye ubora hafifu za QVGA.
Upande wa mbele, kuna kamera kwa ajili ya picha na video yenye uwezo wa kupiga picha zenye ukubwa wa mpaka megapizel 8
Ndani ya Spark 8
Spark 8 inakuja na RAM yenye ukubwa wa GB 2, huku ikiwa na nafasi ya hifadhi yenye ukubwa wa hadi GB 64 ambapo inaweza kuongezwa kwa kutumia microSD. pia ina Helio P22 chipset ambayo ni maboresho ya mtangulizi wake Spark 7 iliyokuwa na Helio A25 chipset.
Simu hii inaendeshwa na mfumo endeshi wa android 11 Go edition ukiwa ndani ya HiOS 7.6. Unaosukumwa betri yenye ukubwa wa 5000mAh yenye kuchajiwa na chaja ya watts 10 kupitia port ya usb. ina uwezo wa kupokea simcrad mbili, 4G LTE, WI-FI, GPS bila kusahau ina sehemu ya kuchomeka earphone (3.5mm audio jack)
Upatikanaji na Bei ya TECNO Spark 8
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, simu hii tayari imeanza kuuzwa nchini Nigeria na kuanzia juma hili itaanza kupatika katika nchi zaidi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Upande wa bei, tarajia kuipata simu hii kwa shilingi za kitanzania 340,000.
Hitimisho
Simu ya Tecno Spark 8 ni simu ya gharama nafuu iliyolengwa kwa watumiaji wenye matumizi madogo mpaka ya kawaida.
Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii na chaneli yetu ya youtube