Rais Samia Suluhu aitaka benki kuu kujiandaa na matumizi ya Sarafu za mtandaoni

Alexander Nkwabi Maoni 144
Mwanza, Tanzania. Rais Samia Suluhu aitaka benki kuu ya Tanzania kujiandaa na matumizi ya Sarafu za mtandaoni (cryptocurrecy/blockchain), kwani huenda ikafika wakati mabadiliko yanayotokea kwingineko yakaingia Tanzania.

Rais ametoa agizo hilo mapema leo wakati akizindua jengo la Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, na kueleza kuwa mabadiliko ya teknolojia na kukua kwa utandawazi kunazidi kuleta mabadiliko mengi, ikiwamo kwenye sekta ya fedha.

Tumeshuhudia kuibuka kwa sarafu mpya kwa njia ya mtandao. Najua bado nchi nyingi ikiwemo Tanzania hazijakubali au kuanza kuzitumia sarafu hizo. Hata hivyo, wito wangu kwa Benki Kuu ni vyema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo. Yakija yakitukamata, yasitukamate hatuko tayari.

“Tumeshuhudia kuibuka kwa sarafu mpya kwa njia ya mtandao. Najua bado nchi nyingi ikiwemo Tanzania hazijakubali au kuanza kuzitumia sarafu hizo. Hata hivyo, wito wangu kwa Benki Kuu ni vyema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo. Yakija yakitukamata, yasitukamate hatuko tayari,” ameagiza Rais Samia

Amesema kutokana na utandawazi, na licha ya kuwa Tanzania haijaruhusu au kuanza kutumia sarafu hizo, wananchi wake wanaweza wakaanza kutumia huko nje ya nchi, na watakaleta jambo hilo nchini, ni muhimu maandalizi yawe yameshafanyika.

Baadhi ya nchi duniani ambazo tayari zimeanza kutumia sarafu za mtandaoni ambazo ni pamoja na Canada, Japan, Marekani, Ufilipino, Ufaransa, Australia, Nigeria.

Bofya hapa kujua mengine mengi kuhusu sarafu za mtandaoni na mengine mengi kuhusu teknolojia.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive