Leo usiku tarehe 14, kutakuwa na Uzinduzi wa iPhone 13 pamoja na bidhaa zingine kutoka kampuni ya Apple. kupitia chapisho hili tunakuelekeza Jinsi ya kufatilia mubashara Apple event kupitia njia mbalimbali. Twende moja kwa moja kwenye njia hizo.
Kupitia YouTube
hii ndio njia rahisi zaidi kutumia popote pale ulipo duniani cha muhimu uwe na mtandao wa internet tu. Unaweza kufalia mubashara kwa kubofya kitufe hapa chini au kwenda YouTube kwenye channel ya Apple.
2. Ukurasa wa Apple Event
unaweza pata tukio zima mubashara kwa kubofya kiunga cha Apple events na moja kwa moja utaweza kutazama tukio hilo
Muda wa kuanza Apple Event
Kwa watazamaji walio Tanzania na nchi za jirani, tukio litaanza kuoneshwa mubashara kuanzia saa mbili kamili usiku za afrika ya mashariki
Tutarajie nini
unaweza soma chapisho letu linaloonesha ni yapi mazuri tunayotarajia kutoka Apple, bofya hapa kusoma chapisho hilo