Apple leo wameachia masasisho makubwa ya mifumo endeshi yake ya simu za iPhone na tableti za iPad yani iOS 15 na iPadOS 15.
Kwenye tukio la uzinduzi wa iPhone 13 la Apple event ilitangazwa kuwa masasisho haya yataachiwa leo jumatatu, katika tukio hilo tuliona pia uzinduzi wa bidhaa zingine mbali na simu za iPhone, ambazo ni pamoja na iPad mpya pamoja na saa janja za Apple Watch Series 7.