Apple leo wameachia sasisho kubwa la mfumo endeshi wa iOS 15 kwa ajili ya simu za iPhone.
Sashisho hili ni bure kabisa kushusha na linazihusu simu zote kuanzia iPhone 6s na kuendelea, vizazi vyote vya iPhone SE pia vitapata sashisho hili bila kusahau toleo jipya la ipod touch. Kwa watumiaji wa iPad wao watapata iPadOs 15 na wale wa Apple watch watapata watchOS 8 leoleo pia.
Hapa chini tunakufafanulia namna ya kuinstall iOS 15 kwenye simu yako ya iPhone, na maelekezo haya pia yanafanana kwenye iPadOS kwa watumiaji wa iPad. Kabla ya yote hakikisha kifaa chako kina uwezo wa kudownload sasisho hili.
Simu gani zitapata iOS 15 au iPadOS 15?
iPhone 12 Mini | iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 5) |
---|---|
iPhone 12 | iPad Pro 11-inch (kizazi cha 3) |
iPhone 12 Pro | iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 4) |
iPhone 12 Pro Max | iPad Pro 11-inch (kizazi cha 2) |
Phone 11 | iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 3) |
iPhone 11 Pro | iPad Pro 11-inch (kizazi cha 1) |
iPhone 11 Pro Max | iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 2) |
iPhone XS | iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 1) |
iPhone XS Max | iPad Pro 10.5-inch |
iPhone XR | iPad Pro 9.7-inch |
iPhone X | iPad (kizazi cha 8) |
iPhone 8 | iPad (kizazi cha 7) |
iPhone 8 Plus | iPad (kizazi cha 6) |
iPhone 7 | iPad (kizazi cha 5) |
iPhone 7 Plus | iPad Mini (kizazi cha 5) |
iPhone 6s | iPad Mini 4 |
iPhone 6s Plus | iPad Air (kizazi cha 4) |
iPhone SE (kizazi cha 1) | iPad Air (kizazi cha 3) |
iPhone SE (kizazi cha 2) | iPad Air 2 |
iPod Touch (kizazi cha 7) |
Jinsi ya install iOS 15 na iPadOS 15
Kabla hujaanza zoezi hili hakikisha simu yako ina chaji ya kutosha, pia hakikisha una data ya kutosha au una chanzo kingine kama Wi-Fi ili kukuharakishia na kukurahisishia mchakato.
Kama kila kitu kiko sawa basi fata hatua zifuatazo;
1. nenda Settings app.
2. halafu chagua General.
3. kisha bofya Software Update.
4. Kwenye kipengele cha Also Available, bofya Upgrade to iOS 15.
5. Chagua Download and install ili kuruhusu mchakato wa ku install kuanza. Unaweza ombwa kuingiza passcode kama unayo.
Fuata maelekezo ili kukamilisha mchakato wa kuinstall. Simu ikimaliza ilo zoezi itajizima kisha kujiwasha. itakapowaka itakuwa na iOS 15. Hatua ni hizi hizi kufuata kama unatumia iPad na unataka kuipa iPadOS 15.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea tovuti ya Mtaawasaba kila siku, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Mtaawasaba kupitia YouTube.
simu ni Iphone Xr ila nashindwaa ku update simu kwa sababu pale kweny install and download haitak kubonyezeka yaan sio ya blue n kijivu kilichofifia .
naomb kujua shida itakuw nini
wanaposema connect your iphone to iTunes on your computer, wana maanisha nini?