Tofauti kati ya simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro

Alexander Nkwabi 1 178
Kufuatia miezi kadhaa ya tetesi kuhusu simu mpya kutoka kampuni ya Google, hatimaye leo tarehe 19, oktoba 2021 simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zimezinduliwa. Simu hizi mbili zinakuja na toleo jipya la mfumo endeshi wa Android 12 na Google kwa mara ya kwanza wana kuhakikishia utapata masasisho ya matoleo ya Android kwa miaka mitano.

Simu hizi mbili simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zinaonekana kama mshindani halisi wa Apple na Samsung kwenye upande wa simu janja sababu kwa mara ya kwanza kabisa Google wametengeneza prosesa iliyopewa jina la Tensor ambayo itakuwa ni mahususi kwa ajili ya simu zao tofauti na awali ambapo walitumia prosesa za Snapdragon. Pamoja na hili simu hizi mbili zinakuja na mambo mengine mengi ya kuvutia. Na kinachovutia zaidi ni bei zake kuwa sio za kutisha ukilinganisha simu kutoka kwenye makampuni mengine zenye hadhi sawa na hizi.

Muonekano

pixel 6 pro 16

Simu ya Pixel 6 ndio inayopeperusha bendera kwa simu za Google kwa mwaka huu. inakuja na maboresho kadhaa ukilinganisha na watangulizi wake. Baadhi ya maboresho ni kama kamera yenye uwezo wa 50MP, sensa ya alama za vidole iliyo ndani ya kioo, betri kubwa, 90hz refresh rate na muonekano wa tofauti ambao unaleta hisia za kumbukumbu za simu kitambo ya Nexus 6P.

Google Pixel 6 Pro ni kubwa kimuonekano kuliko nyenzake, inakuja na kioo kilichojikunja kidogo pembeni chenye ukubwa wa inchi 6.7 chenye uwezo wa 120hz refresh rate ambacho ni gorilla glass victus. Betri kubwa 5000mAh na kamera ya ziada ambayo ni telephoto. Bei yake pia imechangamka kidogo ukilinganisha na mdogo wake Pixel 6. Sifa zaidi za simu zote mbili tunaweza ziona kwenye jedwali chini.

Kamera

pixel 6 pro 10

upande wa kamera, simu za Google zinajulikana kwa kamera kali kwenye soko la simu. Basi tena mwaka huu kama ilivyo jadi yao wamefanya maboresho makubwa upande wa kamera kwa simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro. unaweza kuona sifa za kamera za simu zote hapa chini.

Google Pixel 6Google Pixel 6 Pro
  • 50MP wide yenye EIS na OIS
  • 12MP ultra-wide
  • Laser auto-focus
  • 12MP kamera ya selfie
  • 50MP wide yenye EIS na OIS
  • 12MP ultra-wide
  • 48MP telephoto yenye EIS, OIS, na 4x optical zoom
  • Laser auto-focus
  • 12MP kamera ya selfie

 

Betri

Simu ya Google Pixel 6 Pro inakuja na betri yenye ukubwa 5000Amh, ukubwa ambao hakuna simu yoyote ya pixel imewahi kuwa nao, ambao ni takribani asilimia 7 zaidi ya betri ya Google Pixel 5a ambayo ndio ilikuwa kubwa mpaka ilipotoka pixel 6 pro.

Kwa upande wa Pixel 6, yenyewe inakuja na betri lenye ukubwa wa 4614mAh sawa na Pixel 5a. Sababu kubwa ya kuwa na betri ndogo ni kuwa na kioo chenye resolution ndogo, pia refresh rate ya 90hz ambazo hazitumii chaji nyingi ukilinganisha na mkubwa wake.

Simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zote zina sapoti chaja yenye uwezo wa watt 30 kupitia waya wa USB-C, hata hivyo itakubidi ununue chaja (kama hauna) maana simu zote sasa hawaweki chaja (isipokuwa kwa nchi kama ufararansa ambazo ni lazima simu mpya zije na chaja).

Software

pixel 6 pro 13

Simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zinakuja na toleo jipya la mfumo endeshi wa Android 12 ndani ya boksi, ambapo simu zote mbili zitaweza kupata za masasisho ya mfumo huu kwa miaka mitano, hii inafanya simu kuwa za kwanza kuwezesha jambo hili.

Prosesa ya Tensor

Google Tensor SoC chip 770w 433h

Ukisoma kwenye table hapo chini utaona simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zinatumia prosesa inayojulikana kama Tensor. Tofauti na simu zingine zinazotumia mfumo wa Android ambazo mara nyingi kama sio zote hutumia prosesa za Qualcomm, MediaTek, au Samsung. Prosesa ya Tensor imebuniwa na Gogle wakishirikiana na Samsung na ndiyo itakuwa prosesa yao ya kwanza kwa ajili ya simu zao.

Prosesa hii inafanana kwa kiasi flani na prosesa ya Samsung Exynos 2100 iliyotumika kwenye simu za Galaxy s21. Hii inaingia akilini kwa sababu Samsung wamehusika kwa kiasi kikubwa katika ubunifu mpaka utengenezaji. Hata hivyo Tensor imefanyiwa maboresho kadhaa ili kuongeza uwezo wake wa Artificial Intelligency.

Sifa za simu hizi

Sifa za simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro
Google Pixel 6 Pro
Google Pixel 6
Ukubwa wa kioo6.7-inch LTPO OLED; 3,120×1,440 pixels; 10-120Hz6.4-inch OLED; 2,400×1,080 pixels; 60 or 90Hz
Pixel density512 ppi411 ppi
Upana (Millimita)163.9×75.9×8.9 mm158.6×74.8×8.9 mm
uzito (Gramu)210g207g
Mfumo endeshiAndroid 12Android 12
Kamera50-megapixel (wide), 12-megapixel (ultrawide), 48-megapixel (telephoto)50-megapixel (wide), 12-megapixel (ultrawide)
Kamera ya selfie11-megapixel8-megapixel
uwezo wa kurekodi Video4K 30, 60fps (rear), 4K 30fps (front)4K 30, 60fps (rear), 1,080p 30fps (front)
ProsesaGoogle TensorGoogle Tensor
ukubwa wa hifadhi128GB, 256GB, 512GB128GB, 256GB
RAM12GB8GB
SD cardNoNo
Betri5,003 mAh4,614 mAh
Sensa ya alama za vidolendani ya kioondani ya kioo
KiunganishiUSB-CUSB-C
Inakuja na chaja?HapanaHapana
kitobo cha Headphonendani ya kioondani ya kioo
Sifa maalumu5G sub 6 and mmWave support, Wi-Fi 6E, Ultrawideband, 30W fast charging, Magic Eraser, Motion mode, Real Tone, Face Unblur, Cinematic Pan, 5 years OS and security updates, IP68 rating for dust and water resistance, Gorilla Glass Victus (front and back)5G sub 6 (some carrier models also have 5G mmWave) support, Wi-Fi 6E, 30W fast charging, Magic Eraser, Motion mode, Real Tone, Face Unblur, Cinematic Pan, 5 years OS and security updates, IP68 rating for dust- and water-resistance, Gorilla Glass Victus (front), Gorilla Glass 6 (back)
Bei (TSH)Sh. 2,067,700 (128GB)Sh. 1,377,700 (128GB)

Bei na upatikanaji

Unaweza kuagiza simu ya Google Pixel 6 Pro  kwa bei ya Sh. 2,067,700 kabla ya kodi hii ni ile model ya 128GB na Google Pixel 6 itaipata kwa gharama ya Sh. 1,377,700 pia kwa model ya 128GB.  Zitaingia rasmi madukani kuanzia tarehe 28 oktoba 2021. Simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zinapatikana kwa rangi tatu tofauti: Cloudy White (nyeupe na kijivu), Sorta Sunny (njano na machungwa), and Stormy Black (nyeusi na kijivu). Haijajulikana kama simu hizi zitapatikana kwenye masoko ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, ila ukiagiza unaipata bila shaka yoyote.

Hitimisho

kwenye makaratasi simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro zimeonekana kama ni maboresho ya hali ya juu na imeonesha Google walivoamua kwenda sambamba na makampuni makubwa kama Apple na Samsung. Tusubiri miezi michache ijayo ili tuone uimara na ubora wa simu za Google Pixel 6 na Pixel 6 Pro.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
1
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive