Wiki hii Twitter ili-post feature yake mpya ambayo ipo katika majaribio katika sehemu ya Explore ambayo itakuwa inaonyesha video.
Twitter ni moja kati ya App ambayo nayo pia inatamani kuweka features za TikTok ambayo mwaka huu imepitisha idadi ya watumiaji kuzidi Bilioni 1 kila mwezi. Mtindo wa Video za TikTok umechanganya Instagram na Facebook kutumia Reels, na Snapchat kuweka sehemu ya Spotlights inayofanana na TikTok.
Pia Netflix, YouTube, na Reddit zinapambana kuiga TikTok. Kwa upande wa Twitter unajaribu kuangalia njia nzuri ya kuweka Trending Videos na Video fupi kama sehemu ya contents za Twitter. Japo sometimes Twitter inaacha kuweka features mpya kama ilivyofuta Fleets ambazo zilikuwa zinafanana na Insta Story, WhatsApp Status na Snapchat.