Kampuni ya Google imetoa tangazo katika Game Awards, kuwa mwaka 2022 Android games zote ambazo zinapatikana katika Playstore, zitakwepo zinafanya kazi na kupatikana katika PC zote za Windows 11.
Mwaka huu, Windows 11 ilikuja na uwezo wa kutumia app za Android katika computer. Hiyo ilirahisisha watumiaji wa Windows kuwa na app za Instagram, Snapchat, Twitter n.k katika PC za Windows.
Google Play Games Platform imeshirikiana na Microsoft kuwezesha ushirikiano huo.
Watumiaji wa Windows watakuwa na uwezo wa ku-download na kucheza games za Android. Wataweza kuunganisha akaunti moja na kuwezesha watumiaji kuendelea na games za simu katika PC kwa akaunti moja na kuendelea kucheza games katika PC kwa akaunti moja.
Ni strategy ya Microsoft na Google kukuza soko la apps na games za Android katika PC za Windows.