Google wameachia toleo jipya mfumo endeshi wa Android 13 Beta 1 siku ya Jumanne kwa baadhi ya simu za Pixel kwa ajili ya ma developer na watu wengine kuufanyia majaribio kabla sasisho la mwisno halijatoka. Hadi sasa Google wamesema toleo hili la Android 13 litajikita zaidi katika kuboresha faragha na usalama.