Android 15 inakuja na uwezo wa kutuma ujumbe kwa satelaiti, NFC iliyoboreshwa na zaidi…

Mtaawasaba Maoni 152

Google hivi karibuni imetoa toleo la pili la Android 15 kwa wasanidi wa programu, katika toleo hili tunaona vipengele mbalimbali vya kusisimua na maboresho ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutuma ujumbe wa satelaiti na zaidi. Toleo hili la wasanidi hutumika kama uwanja wa majaribio kwa vipengele vinavyokuja ambavyo vinaweza kujumuishwa katika toleo la mwisho la umma baadaye mwaka huu. Katika makala hii, tutachunguza nyongeza muhimu zilizoletwa katika toleo hili, ikiwa ni pamoja na uwezo wa muunganisho wa satelaiti, maendeleo katika malipo yasiyo na mawasiliano, utambuzi wa lugha nyingi, uthabiti wa sauti, na mwingiliano na PDF kupitia programu.

 

Uwezo wa kutuma ujumbe kwa njia ya Satelaiti

Moja ya vipengele vilivyokuwa vinasubiliwa kwa hamu sana ni uwezo wa kutuma ujumbe kwa njia ya satelaiti. Kupitia maboresho haya mapya, simu zinazotumia mfumo endeshi wa Android zitaweza kutumia mfumo huu wa muunganisho kupitia satelaiti kwa matumizi mbalimbali. Mojawapo ni uwezo wa kutuma ujumbe hata ukiwa kwenye maeneo yenye shida ya mtandao.

 

Huduma za NFC na njia za malipo zilizoboreshwa

Android 15 inalenga kuboresha namna mtumiaji ataweza kufanya malipo kwa urahisi. Sasa utaweza kufanya malipo kwa kubofya mara moja kwenye simu yako kwa kutumia teknolojia  ya NFC (Near Field Communication) iliyoboreshwa zaidi. Programu zinazotumia mfumo wa NFC sasa zitaweza kutoa taarifa kwa mtumiaji iwapo watakuwa wanarekodiwa, hii itaongeza usalama zaidi na uwazi zaidi katika mchakato mzima wa kufanya malipo.

 

Utambuzi wa lugha nyingi zaidi ulioboreshwa

Android 15 inaongeza maboresho kwenye huduma ya utambuzi wa lugha mbalimbali ili kuleta urahisi kwa watumiaji hasa wanapohitaji kubadili lugha moja kwenda nyingine au kutafsiri. Maboresho haya ambayo yalionekana kwa mara ya kwanza kwenye Android 14, yanazidi kuongezwa zaidi kwenye toleo hili jipya.

 

Maboresho zaidi kwa simu zinazojikunja

Wasanidi wa programu wanapewa uwezo zaidi kucheza na skrini ndogo upande wa nje kwenye simu zinazojikunja. Hii inamaanisha vioo vya nje kwenye simu zinazojikunja vitaweza kuwekwa taarifa zaidi na kuongeza urahisi kwa watumiaji kwani wasanidi wataweza kutengeneza programu ambazo zitaweza kufanya kazi vizuri kwenye simu zinazojikunja.

 

Maboresho kwenye vipengele vya mafaili ya PDF

Google imefanya maboresho zaidi kwenye vipengele vya mafaili ya PDF kwenye programu za Android. Kwenye toleo la pili la wasanidi la Android 115, app zinaongewa maboresho kwenye mafaili yenye nywila, attonation, uwezo wa kuhariri fomu, kutafuta, na kunakili. Maboresho haya ya PDF yatafanya matumizi ya mfumo endeshi wa Android kuwa rahisi zaidi.

MADA: ,
Mwandishi Mtaawasaba Msimamizi wa Mfumo
Mitandao ya Kijamii
Mtaawasaba inakuletea habari za teknolojia, uchambuzi na makala kuhusu teknolojia mbalimbali ikiwemo simu za mkononi, tableti, kompyuta, programu na mengineyo mengi yahusuyo teknolojia.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive