Google yabadili jina la Android Wear kuwa Wear OS ili kuvutia watumaji wa iPhone zaidi

Alexander Nkwabi Maoni 152
Mfumo endeshi wa Android ambao ni mahususi kwa ajili ya Saa janja unaojulikana kama Android Wear umebadilishwa jina na kuwa Wear Os by Google. Hayo wameandikwa kwenye blog ya Google na Dennis Troper ambaye ni Director wa bidhaa ya Android wear (kabla haijabadilishwa jina) na kuwa Wear OS by Google.

wear os

Sababu kubwa ya kubadili jina la mfumo endeshi huu sio nyingine bali ni kuwateka zaidi watumiaji wa iPhone, hii inakuja baada ya taarifa kuonesha kuwa Android wear imekuwa ikitumika na takribani moja ya tatu ya watumiaji wa iPhone kwa mwaka jana pekee. Android wear ilianza ku support iPhone mwaka 2015,

Google wameongeza kuwa mnamo msimu wa sikukuu za mwaka jana wameweza kuona ongezeko la manunuzi ya bidhaa zenye Android Wear kwa Asilimia zipatazo 60. Hata hivyo soko la Saa janja bado linashikiliwa na kampuni kama Apple, Fitbit, Xiaomi, and Garmin ambazo zote hazitumii mfumo endeshi huo wa Android Wear.

Watumiaji wa Saa janja zenye Wear Os wataanza kuona mabadiliko ya jina na muonekano kwenye saa janja zao na app kwenye simu zao kuanzia majuma machache yajayo

Mabadiliko ya jina yanamaanisha mabadiliko na kutiliwa mkazo kwa mfumo endeshi huu ambao mpaka sasa kampuni za saa janja zimeweza tengeneza saa janja za aina tofauti zaidi ya 50 zenye kutumia mfumo endeshi huo. Google wameahidi mambo makubwa zaidi yanakuja kwenye mfumo endeshi huu.

Saa janja zinakusaidia kusimamia na kufatilia mienendo yako ya mazoezi na afya kwa ujumla, pia zinaweka karibu na watu wa muhimu katika maisha yako bila kusahau uwezo kukupa taarifa za muhimu kwa haraka bila kugusa simu yako.

Google wametoa orodha ya saa janja ambazo zitapata mfumo endeshi huu uliobatizwa jina jipya. Ambapo mpaka sasa ni saa 33 zikiwemo:

  • Casio PRO TREK Smart WSD-F20
  • Casio WSD-F10 Smart Outdoor Watch
  • Diesel Full Guard
  • Emporio Armani Connected
  • Fossil Q Control
  • Fossil Q Explorist
  • Fossil Q Founder 2.0
  • Fossil Q Marshal
  • Fossil Q Venture
  • Fossil Q Wander
  • Guess Connect
  • Gc Connect
  • Huawei Watch 2 (both cellular & non-cellular versions)
  • Hugo BOSS BOSS Touch
  • Kate Spade Scallop
  • LG Watch Sport
  • LG Watch Style
  • Louis Vuitton Tambour
  • Misfit Vapor
  • Michael Kors Access Bradshaw
  • Michael Kors Access Dylan
  • Michael Kors Access Grayson
  • Michael Kors Sofie
  • Montblanc Summit
  • Movado Connect
  • Mobvoi Ticwatch S & E
  • Nixon Mission
  • Polar M600
  • Skagen Falster Smartwatch
  • TAG Heuer Connected Modular 41
  • TAG Heuer Connected Modular 45
  • Tommy Hilfiger 24/7 You
  • ZTE Quartz

Endelea kuwa nasi @Mtaawasaba ili tuendelee kukupa habari, makala na uchambuzi wa mambo mbalimbali ya teknolojia kadri yanavotoka, na pia usisahau kutufuata katika Social network mbali mbali kwa jina la mtaawasaba, Pia usisahau kusubscribe kwa barua pepe kuweza kupata habari mpya kila zinapoingia, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini! Ahsante sana

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive