iPhone 15 hatimaye inaweza kuja na chaja ya USB-C

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mchambuzi Ming-Chi Kuo, iPhone 15 hatimaye inaweza kuja na chaja ya USB-C badala ya lightining kama ilivyozoeleka. Habari hii inadaiwa kutoka kwa vyanzo vya usambazaji na utabiri wake mara nyingi huwa kweli.

Apple kila mwaka ina uvumi wa iPhone mpya kuja na chaja ya USB-C. Uvumi huu umekuwepo tangu 2017 . Kuo mwenyewe ametabiri mara kadhaa miaka ya nyuma.

Kama habari hii itakuwa ya kweli basi iPhone 14 ndiyo itakuwa ya mwisho kutumia chaja ya lightining. Kwa sasa Vifaa vingi vya Apple vinatumia USB-C huku zikiwa zimebaki flagship ya iPad, Airpods na iPhone.

IPhone 15 itafaidika kwa njia mbalimbali kutokana na kupitishwa kwa USB-C – kuchaji haraka na muunganisho mpana zaidi, hasa kwa vifaa vya Apple vinavyotumia USB-C. 

Maelezo mengine yanadai Apple wanalazimika kuhamia USB-C kwenye bidhaa zake baada ya nchi za umoja wa Ulaya kupitisha sheria itakayotaka bidhaa zote za kieletroniki zitakazouzwa kwenye nchi za umoja huo kuwa na chaja moja inayofanana kwa bidhaa zote, na imependekezwa matumizi ya USB-C

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive