Mambo 6 unayotakiwa kujua kuhusu iPhone SE (2022)

Mwandishi Diana Benedict

Baada ya tetesi nyingi mwezi mzima uliopita hatimaye leo kupitia Apple Event ilopewa jina Peek Performance, Apple wamezindua bidhaa mpya kadhaa ikiwemo simu ya “gharama nafuu” ya iPhone SE 2022 kizazi cha tatu, simu yenye nguvu na muonekano wa zamani ikiwa na uwezo mkubwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na simu zingine za iPhone. Simu hii inakuja na mfumo endeshi wa iOS 15.

Muonekano wa iPhone SE

Simu hii mpya inakuja na muonekano unaofanana kwa karibu sana na vizazi viwili vilivyoitangulia vya iphone SE huku ikibakiza kitufe maarufu kama home button. Ukubwa wa simu ni inchi 4.7 na kioo cha Retina HD chenye teknolojia ya LCD kikiwa na refresh rate ya 60HZ

Simu hii inakuja na rangi mbili unazoweza kuchagua ambazo ni Midnight na Starlight. Upande wa nyuma kuna kioo kigumu kinachofanya simu iwe ngumu kuvunjika. Simu hii inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi kuingia ikiwa imethibitishwa na IP67.

Muonekano wa iphone se

Prosesa na mfumo Endeshi wa iPhone SE

Simu hii inakuja na prosesa ya A15 Bionic sawa na inayopatiakana kwenye simu ya iPhone 13. Katika kipengele hiki tunaona maboresho makubwa ukilinganisha na waanguliza wake. Prosesa hii inatosha kabisa kusukuma mfumoendeshi wa iOS 15.4 ambao utakuwezesha shuguli za kupiga picha na video kuwa kwa ulaini. Pia simu hii ina uwezo wa Wi-Fi 802.11, Bluetooth 5.0 bila kusahau uwezo wa  5G na mifumo mingine ya nyuma.

A 15 bionic

Kamera ya iPhone SE

Kama ilivyokuwa kwa matoleo ya nyuma, simu hii inakuja na kamera moja upande wa nyuma yenye lenzi ya 12-megapixel wide-angle. ambapo itakuwa na uwezo wa kupiga  portrait mode na uwezo kurekodi mpaka 4K, Slomo na time lapse. Upande wa kamera ya Selfie ni 12MP Wide na inaweza kurekodi video ya 1080p kwa frame 30 mpaka 120 kwa sekunde

Kamera ya iphone se

RAM na Hifadhi ya iPhone SE

Simu hii inakuja na matoleo mawili ambapo moja itakuwa na RAM 3GB na 4GB ambayo itakuwa na hifadhi ya 128GB huku kutakuwa na yenye 256GB yenye 3GB. Simu hii inakuja na sensa ambazo ni TouchID (Home Button), accelerometer, proximity, gyro, compass, na barometer.

Iphone se 2022

Betri ya iPhone SE

Simu hii inakuja na betri yenye uwezo wa kuchaji kwa haraka mpaka 18W (inafikisha asilimia 50% kwa dakika 30). Kama simu zingine za Apple, inakuja na charging port yenye kuruhusu Lightning cable, pia ina teknolojia ya USB 2.0

Bei na Upatikanaji wa iPhone SE

Simu hii inataanza kupatiakana kuanzia mwezi wa 3 tarehe 18, ila unaweza ku pre order kuanzia ijumaa tarehe 11 mwezi wa tatu. Bei ya kuanzia ni shilingi za kitanzania milioni 1 bila kodi. Mpaka sasa haijajulikana ni lini na kwa gharama kiasi gani itauzwa Tanzania

Avatar of diana benedict
Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive