Kiwanda cha Simu za Mkononi kuzinduliwa Zanzibar

Mwandishi Diana Benedict

Siku chache zijazo Zanzibar inatarajia kujenga Kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza simu za mkononi na kusaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa visiwa hivyo.

b10c571740b47170003b36b48ed49648b91ad08a376d434118afc46496b2ed5a

Kutoka katika Gazeti la habari leo la Machi 8 2017 zilisema Kiwanda hicho kitakachoanzishwa hivi karibuni na Kampuni ya U$I ya kutokea Korea ya Kusini, kitaanza kwa kuunganisha vifaa vya simu na baada ya miaka minne kuanza kutengeneza simu kamili.

Kiwanda hicho kwa sasa kitaanza na kkunganisha simu na vifaa va simu na hapo baadae kuazamiwa kuengeneza simu kamili.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud Alisema kiwanda hicho anachodhani hakuna katika nchi za Afrika Mashariki, kitaanza kwa kuajiri watu 60 hadi 120 kwa kuanzia. Lakini, alisema kwa mtazamo wa wawekezaji, kitaanza uzalishaji wa simu kamili baada ya miaka minne. Alisema kabla ya muda huo, watatoa fursa kwa vijana 10 kutoka Zanzibar kupata mafunzo ya ziada katika maeneo ya uzalishaji simu na kupata shahada za uzamili na uzamivu kwenye teknolojia hiyo, hivyo kuzalisha simu kutoka mkoa huo.

Na pia aliongeza na kusema kwa sasa kuna viwanda vya uzalishaji maji, viwanda vidogo vya nguo, usindikaji wa lami Fumba na kuna kiwanda kinaanza Nyamanzi, kujenga nyumba. Kiwanda hicho kina uwezo wa kujenga nyumba ya kawaida kwa siku tisa.

Mkuu wa mkoa Ayoubu aliendelea na kusema katika uchumi wa viwanda, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameagiza kuwa katika kila mkoa katika visiwa hivyo vya zanzibar, kila wilaya iwe na kiwanda cha mkakati angalau kimoja na sasa wanaendelea kubainisha maeneo ya viwanda hivyo kujengwa. Kwamba katika mkoa wake, kwa sasa wanaangalia aina ya viwanda vya kuanzisha na upatikanaji wa rasilimali, kwani maeneo mengi yametumika kwa makazi na yaliyobaki yanatumika kwa kilimo cha mazao ya viungo mbalimbali.

Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii hapo chini na endelea kufuatilia habari kutoka mtaawasaba.com, Pia usisahau kusubscribe katika chanel yetu ya Youtube kupata habari zaidi za teknolojia kila wiki.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive