Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii hasa Twitter utakuwa unajua ugumu ya kuelezea hisia zako kwa herufi 140 pekee. Sasa kampuni ya Twitter inafanya majaribio ya kuongeza idadi ya herufi mpaka 280, kama majaribio haya yatafanikiwa tutaona mabadiliko makubwa katika namna ambayo watu wana twiti.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Twitter imeongeza idadi ya herufi kwa lugha zote isipokuwa kijapani, kichina na kikorea, ambapo wanasema imekuwa changamoto kwa watu kuelezea hisia zao kwa herufi izo 140 za awali, tatizo ambalo limeonekana sana hasa baada ya Twitter kupata umaarufu mkubwa.
Meneja wa bidhaa Aliza Rosen ameandika katika blogu ya kampuni kuwa; lugha za bara Asia zilizo tajwa hapo juu hazitapata mabadiliko kutokana namna maandishi yake yalivyo.
“Utafiti wetu umeonesha kuwa ukomo wa herufi umekuwa tatizo kubwa kwa watumiaji wa lugha ya kiingereza kuliko wale wanaotwiti kwa kijapani,” ameeleza Rosen.