Meta kusitisha bidhaa zake za Portal na kufuta saa janja 2 ambazo hazijatoka

Mwandishi Amos Michael

Ni siku chache tangu Meta kutangaza kuwa itapunguza wafanyakazi takribani 11,000 ambao ni sawa na asilimia 13 ya wafanyakazi wote kwenye kampuni ya Meta. Leo kumekuja habari kuwa Meta kusitisha bidhaa zake za Portal na kufuta saa janja 2 ambazo hazijatoka.

Ripoti hii imekuja kupitia Reuters na kuchapishwa na mtandao wa TheVerge ikifafanunua kusitishwa kwa bidhaa hizo mbili na kampuni ya Meta

Mnamo Juni, Meta ilitangaza kuwa haitazalisha tena vifaa vya Portal kwa watumiaji. Na kwa kuongezea, chapa hiyo ilisema haitatoa tena saa janja zilizopewa jina “Milan.” Kulingana na ripoti, saa janja hizi zilipangwa kuwasili mnamo 2023. Na zilitarajiwa kuingia sokoni kwa bei ya dola za marekani 350 na zitajumuisha kamera mbili zilizojengwa kwa ajili ya simu za video. Sasa, kampuni hiyo imefanya uamuzi mwingine wa kuachana na mipango yake ya kuzindua saa zake janja.

Kifaa cha Facebook Portal ni onyesho mahiri (smart display) ambayo lengo lake kuu ni kupiga simu za video kwa marafiki na familia kupitia huduma ya kupiga simu ya video iliyojengwa ndani ya Facebook Messenger, lakini Facebook Portal pia inajivunia utendaji wa Alexa.

Portla

Portal ambayo ilizinduliwa mwaka 2018, kumekuwa na matoleo mapya kadhaa huku Portal Go ikiwa ndio toleo jipya kabisa lililoachiwa na Meta. Hata hivyo bidhaa hii imeshindwa kuvutia watumiaji wa kawaida moja ya sababu kubwa ni kuhusu sera za Faragha za Facebook. Pia sababu nyingine kubwa ni ushindani kutoka kwa bidhaa kama Amazon Echo, na baada ya kujaribu kwa miaka kadhaa hatimaye Meta wame “sarenda”.

Mpaka sasa haijaeleweka ni kwanini Meta wamesitisha uuzaji wa bidhaa yake ya Portal na kusitisha saa janja hizo mbili zilizotarajiwa kutoka hivi karibuni.

 

 

Avatar of amos michael
Mwandishi Amos Michael Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Meezy ni mchangiaji wa machapisho mbalimbali hapa Mtaawasaba tangu kuanzishwa kwake. Meezy ni mpenzi wa Android na anapokuwa nyumbani hupendelea kupiga kinanda na kuandaa muziki
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive