Netflix imepoteza Wateja 200,000, Kuja na mpango wa Matangazo

Mwandishi Emmanuel Tadayo
#link=%7B%22role%22:%22standard%22,%22href%22:%22https://www.netflix.com/%22,%22target%22:%22%22,%22absolute%22:%22%22,%22linkText%22:%22Netflix%22%7D" target="_blank" rel="noopener noreferrer nofollow" data-component="externalLink">Netflix imepoteza wateja 200,000 katika robo ya kwanza ya mwaka 2022, hii ni mara ya kwanza kwa idadi kubwa ya wateja kushuka kwa miaka 10. Kwa mujibu wa ripoti, inatarajia kupoteza wateja milioni 2 zaidi katika miezi mitatu kutoka Aprili hadi Juni, kampuni hiyo ilisema Jumanne.

Katika ripoti yake ya mapato ya robo ya kwanza, Netflix imesema sababu kubwa ya kushuka kwa wateja ni vita kati ya Urusi na Ukraine ambapo walisitisha huduma nchini Urusi na hivyo kupoteza wateja takribani laki 7. Pia sababu ingine inatajwa kuwa ni watumiaji wengi kuchangia password.

Mpango wa Netflix kuokoa jahazi

Katika ripoti ya mapato  robo ya kwanza, Netflix imefafanua kuwa zaidi ya watumiaji milioni 100 wanachangia password kwenye akaunti zao za Netflix, kuchangia password kumetajwa kama sababu moja wapo ya kushuka kwa wateja wake. Ili kukabiliana na jambo hili,

Netflix Kulipisha Zaidi Wanaochangia Password

Tayari Kipengele hicho kinafanyiwa majaribio kwa watumiaji nchini Chile, Costa Rica, na Peru, wamedai hii ni njia ya Netflix kupambana na kuchangia password na kupata wanachama zaidi, kwa kuzingatia watu wanaotumia Netflix bure sio wanachama kweli. Kipengele hicho kitafikia masoko zaidi katika mwaka mmoja.

Njia nyingine Netflix inakusudia kutatua shida ya kupungua kwa wateja ni kwa kuanzisha mipango ya bei rahisi, pamoja na kuweka matangazo hivi karibuni. Mpango huu wa matangazo haukuwa mkakati wa awali lakini imeonekana wazo hili litaongeza wateja zaidi na mapato.

Netflix imetaja sababu zingine za kupungua kwa watumiaji ni pamoja “matumizi ya TV zilizounganishwa,” na huduma pinzani kama Disney+ na Amazon, gharama za data, vita vya Urusi na Ukraine, kuongezeka kwa mfumuko wa bei, pia wamesema COVID-19 pia imechangia.

Netflix inapanga kutatua suala hili na hatua zilizotajwa hapo juu  kwa kuongeza maudhui bora. Na bado, wanatarajia upotezaji wa wateja karibu milioni 2 katika robo ya pili ya 2022.

Unafikiria nini kuhusu Netflix kupoteza wateja? Je, unadhani imeanza kupoteza mvuto wake? Shiriki mawazo yako katika sehemu ya maoni hapa chini.

 

 

 

 

 

 

Avatar of emmanuel tadayo
Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive