Bodi ya wakurugenzi wa kampuni inayotengeneza semiconductor ya Qualcomm kwa pamoja wagomea dili ya dola za kimarekani billioni 121 kununuliwa na kampuni ingine inayotengeneza semi conductor ya Broadcom
Katika maelezo yao mbele ya waandishi wa habari, bodi ya wakurugenzi wa Qualicomm ilisema kuwa kiasi cha dola 82 kwa shea kilikuwa hakitoshi na kiliishushia thamani ( japo kama ingekubalika basi ingekuwa ni dili kubwa kuliko yote kuwahi kutokea ulimwengu wa elektroniki.)
Broadcom walisema ofa hii ni kubwa na ya mwisho, baada ya kuongeza asilimia 15 ya ofa yao ya mwanzo iliyotangazwa mapema mwezi ya kumi na moja 2017 ambayo ilikataliwa, ilikuwa ni ya dola za kimarekani billioni 105. Akizungumza na gazeti la New York Times, Mkurugenzi mtendaji wa Broadcom, bwana Hock Tan alisema ofa kama hii ilitakuwa kukubaliwa na bodi yoyote.
Broadcom ambayo kwa sasa makao makuu yake ni Singapore ina mpango wa kuhamishia makao makuu yake nchini Marekani baada ya bwana Tan kuonana na raisi wa Marekani Donald Trump kwenye ikulu ya White House.
Kama Qualcomm ingekubali kununuliwa na Broadcom ingeifanya kampuni hiyo kuwa kampuni kubwa ya tatu duniani kwa utengenezaji wa semiconductor nyuma ya Intel na Samsung electronics. Muungano wa kampuni izo mbili ungewezesha utengenezwaji wa vifaa ambavyo ningetumika kutengeneza simu janja zaidi ya bilioni moja kila mwaka.
Ofa hii imekuja wakati kipindi kigumu kwa Qualcomm ambayo imekumbwa na mgogoro mkubwa kisheria na kampuni ya Apple ambapo Qualcomm imeadhibiwa na Umoja wa Ulaya faini ya dola za kimarekani billioni 1.2 baada kugundulika kuwa walikuwa na lengo la kuwazuia wapinzani wao kama intel kufanya kazi. Qualcomm wamesema watakata rufaa kuhusiana na faini hiyo.
Hisa za Qualcomm hivi karibuni zimekuwa zikishuka thamani baada ya ripoti kuwa Apple inataka kuachana nao na kufanya kazi na kampuni pinzani ya intel badala yake.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Mtaawasaba, pia usisahau ku subscribe kama bado hujafanya hivyo ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka kila zinapotoka tu.