Kila kitu unachotakiwa kujua kuhusu Samsung Galaxy S22 na S22 Plus

Diana Benedict Maoni

Leo Tarehe 9 Februari 2022 katika tukio la Galaxy unpacked 2022 Kampuni ya Samsung imezindua Simu tatu mpya ambazo ni Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus pamoja na Galaxy S22 Ultra (ambayo imechambuliwa kwenye chapisho lingine). Mtaawasaba imefanya uchambuzi wa kina katika simu hizi mbili za Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus ambapo tutaangazia sifa, muonekano, bei na vitu vipya vilivyoongezeka na mabadiliko mengine katika simu hizi mbili.

Muundo na kioo wa Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus

samsung galaxy s22 mbele

Kimuonekano Simu zote mbili zina muonekano wa kufanana isipokuwa ukubwa. Mwaka huu Samsung wamebadili kidogo kwa kuacha kutumia plastiki upande wa nyuma na simu zote zilizozinduliwa kuja na kioo upande wa nyuma na upande wa pembeni kuzungukwa na metali.

Samsung Galaxy S22 na S22 plus hazina uwezo wa kutumia S Pen ambapo simu ya S22 Ultra ndio imepewa uwezo huo pekee kama mbadala wa Note ambayo imeuliwa kuanzia mwaka huu.

Kioo cha S22 ni kidogo kiasi ukilinganisha na mtangulizi wake S21. simu hizi mbili zinakuja na kioo chenye ukubwa wa inchi 6.1 kwa s22, na inchi 6.6 kwa s22 plus ambayo ni ndogo kidogo kuliko Galaxy S21 ambayo ina ukubwa wa inchi 6.2, na S21 Plus ilikuja na ukubwa wa inchi 6.7.

Galaxy S22 inakuja na upana wa (146×70.6×7.6mm) ambao pia ni mdogo kuliko mtangulizi wake S21. Kupungua huku sio kwa kawaida ukilinganisha mtiririko wa ongezeko la ukubwa kwa simu zilizotoka awali

 

Kamera za Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus

Galaxy S22 na Galaxy S22 Plus

Galaxy S22 and S22 Plus zinakuja na kamera tatu, ya kwanza ni 50mp wide lenzi, ya pili ni 12mp ultrawide na 10mp telephoto kamera.

Kulikuwa na tetesi zilizosema kuwa Galaxy s22 zitakuja na kamera zenye uwezo wa 200mp ambao ndio ungekuwa uwezo mkubwa kabisa kutokea kwa sasa, haikuwa hivyo labda kwenye matoleo yajayo

Mfumo endeshi , Betri na ufanyaji kazi wa Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus

Galaxy-S22

Simu zote mbili zinakuja na prosesa mpya na yenye nguvu kabisa ya Qualcomm Snapdragon 8 kizazi cha 1 ukilinganisha s21 na s21 fe iliyokuja na Snapdragon 888. simu zenye prosesa hii ni kwa ajili ya soko la marekani tu, kwa wengine wote waliobakia simu zitakuja na prosesa ya exynos inayotengenezwa na Samsung wenyewe.

Kwenye box hakuna chaja, itakubidi ununue chaja kama huna, nunua chaja yenye uwezo wa watt 45 kwa s22 plus na watt 25 kwa s22 plain. Ukubwa wa betri umepungua kwa simu zote mbili ambapo s22 inakuja na betri yenye ukubwa 3,700mAh na s22 plus inakuja 4,500mAh, hii inatokana na kupunguzwa kwa ukubwa wa simu zenyewe. Je, zitaweza kweli kukaa na chaji kama watangulizi wake?

Simu zote zinakuja na mfumo endeshi wa Android 12 ikiwa imefunikwa na ngozi ya OneUi kutoka Samsung.

Sifa za Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus

Unaweza kuona Specification zote za simu hizi mbili kupitia chati hii:

SAMSUNG GALAXY S22 VS. S22 PLUS

KipengeleGalaxy S22Galaxy S22 Plus
Mfumo EndeshiAndroid 12Android 12
Kioo6.1-inch OLED6.6-inch OLED
Ukubwa wa picha1080×23401080×2340
Refresh rate120Hz120Hz
Upana70.6 x 146 x 7.6 mm75.8 x 157.4 x 7.6 mm
Uzito168g196g
Betri3,700mAh4,500mAh
ProsesaSnapdragon 8 Gen 1 CPUSnapdragon 8 Gen 1 CPU
RAM8GB8GB
Hifadhi128GB, 256GB128GB, 256GB
Kamera ya nyuma50MP (f/1.8) wide, 12MP (f/2.2) ultrawide, 10MP (f/2.4) telephoto50MP (f/1.8) wide, 12MP (f/2.2) ultrawide, 10MP (f/2.4) telephoto
Kamera ya mbele10MP10MP
video (kamera ya mbele)4K  60fps4K  60fps
video (kamera ya nyuma)8K  24fps, 4K 60fps8K  24fps, 4K  60fps
MatunduUSB-CUSB-C
S Penhapanahapana
UsalamaUltrasonic fingerprint sensor, facial recognitionUltrasonic fingerprint sensor, facial recognition
ulinzi dhidi ya vumbi na majiIP68IP68
UWBhapanandiyo
uwezo wa kuchaji bila wayandiyondiyo
Uwezo waWireless5G mmWave / sub-6GHz, LTE, Wi-Fi 6, Bluetooth 5.25G mmWave / sub-6GHz, LTE, Wi-Fi 6E (6Ghz), Bluetooth 5.2
Bei ya kuanziaTsh 1,850,000Tsh. 2,300,000

 

Bei, Upatikanaji wa Samsung Galaxy S22 na Samsung Galaxy S22 plus

Samsung Galaxy S22 Inatarajiwa kuuzwa kati ya Dola za kimarekani 800 sawa na Shilingi za kitanzania 1,850, 000/= na Samsung Galaxy S22 Plus inatarajiwa kuuzwa kati ya dola za kimarekani 1000 sawa na Shilingi za kitanzania, 2,300,000/=, Japo hizi ni bei zilizotangazwa ila kwa sasa haijathibishishwa Tanzania Zitauzwa Shilingi ngapi.

Tupe maoni yako kuusu na simu hizi mbili kwenye sehemu ya comment hapo chini. Pia Endelea kuwa nasi kujua zaidi kuhusu uchambuzi wa simu na mambo mengine ya teknolojia, Pia usisahau kutufollow kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, facebook na Instagram.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako