Habari njema kwa watumiaji wa simu za Android wa Kenya, sasa hawahitaji kuwa na kadi za benki ili waweze kununua app, filamu au manunuzi mengine kupitia Google playstore kwani Google wameongeza njia ya malipo ya M-Pesa Express.
Safaricom ambao ndio watoa huduma ya M-Pesa kenya wameungana na DOCOMO Digital katika kulifanikisha hili kwa kutumia API ya mfumo wa malipo ya Google Play, inayowaruhsu watumiaji wa M-Pesa kulipia bidhaa na huduma kutoka kwenye duka hilo. Hii ni ndoto iliyotimia kwa watumiaji wengi ambao walitamani kununua app au huduma zingine ila mfumo mzima haukuwa rafiki.
Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa huduma hii, Mkurugenzi wa mipango wa Safaricom bwana Joseph Ogutu alisema, “muungano ni jambo zuri katika kurahisisha huduma kwa wateja wetu. Muungano huu unawawezesha wateja wetu kuongeza machaguo kwenye malipo wanapojuwa wakitumia Google Play”
Endelea kuwa nasi @Mtaawasaba na pia usisahau kutufuata katika Social network mbali mbali kwa jina la mtaawasaba, Pia usisahau kusubscribe email kuweza kupata habari mpya kila zinapoingia, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini! Ahsante sana