Tovuti ya iCloud ya Apple yapata muonekano mpya, inavutia zaidi.

Mwandishi Diana Benedict
Highlights
  • Muonekano wa iCloud kwa muda sasa umeonekana kupitwa na wakati, huku ukiwa na muonekano wa maleo ya nyuma ya iOS. Hatimaye Apple wameamua kufanya mabadiliko makubwa kwa upande wa muonekano na ni ya kuvutia sana.

Tovuti ya iCloud ni muhimu ikiwa unataka kufikia haraka baadhi ya programu au huduma ambazo zipo kwenye Mac, iPhone au iPad yako, haswa ikiwa uko kwenye kompyuta usiyomiliki au unatumia PC (yenye mfumo endeshi wa Windows au mifumo isiyo ya Apple).

Muonekano wa iCloud kwa muda sasa umeonekana kupitwa na wakati, huku ukiwa na muonekano wa maleo ya nyuma ya iOS. Hatimaye Apple wameamua kufanya mabadiliko makubwa kwa upande wa muonekano na ni ya kuvutia sana.

Muonekano mpya wa tovuti ya iCloud ambao umeanza rasmi jumatano hii, na kila mtu anayetembelea tovuti hii kuanzia sasa ataweza kuona mabadiliko. Muonekano huu mpya ambao ni vigae (kama ambavyo viko kwenye matoleo mapya ya iOS) ambavyo kila kimoja kina huduma fulani ikiwemo Barua, Picha, Kurasa na zingine zaidi.

Unaweza kubadili mpangilio wa vigae kwenye ukurasa wa mwanzo kadri upendavyo kama huduma ya barua au picha kuwa sehemu unayotaka mwenyewe.

Kuna alama ya kujumlisha upande juu kulia mwa skrini ambapo ukigusa alama hiyo utapata machaguo yakiwemo kuanzisha barua pepe mpya, notes, kalenda, matukio na kumbukumbu. Au unaweza kubofya ili kutengeneza kurasa mpya, namba na zaidi.

Pia kuna chaguo la menyu litakalokuwezesha kusimamia vipengele vya iCloud+ kama vile Hide My Email, iCloud Private Relay na HomeKit Secure Video.

Chini kabisa ya ukurasa kuna taarifa kuhusu mpango wa hifadhi yako ya iCloud kama vile umetumia hifadhi kiasi gani. Pia kuna kipengele cha data recovery kurudisha mafaili yako, bookmarks, majina na kalenda uliyofuta.

Je, umeshaanza kutumia muonekano huu mpya wa iCloud? Ningependa kusikia kutoka kwako, acha maoni yako kwenye kipengele cha maoni hapo chini.

Pia usikose Kutembelea Mtandao Wako Wa Mtaawasaba Kila Siku na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili uednelee kuwa mbele kwenye maswala ya teknolojia.

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive