Mamlaka ya mapato Tanzania TRA na kampuni ya Meta wajadiliana kuhusu kodi

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA na kampuni ya Meta wajadiliana kuhusu kodi. Kupitia kwa Mkurugenzi wake wa huduma na elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa ufafanuzi baada ya TRA kukutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini Tanzania.

TRA leo Aprili 21, 2022 imetoa taarifa fupi kupitia ukurasa wake wa Twitter,  ikieleza kufanya mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.

#DARESSALAAM Timu ya Wataalam wa Kampuni ya @meta inayomiliki mitandao ya @facebookapp @instagram pamoja na @whatsapp leo 21 Aprili, 2022 imefanya mazungumzo ya awali na TRA kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam. pic.twitter.com/PmqbA69nD2

— TRA Tanzania (@TRATanzania) April 21, 2022

“Mkutano kati ya TRA na kampuni ya META ulikuwa ni mkutano wa awali wao kuweza kuelewa mazingira ya sheria za kodi za Tanzania na pia kuweza kutupitisha katika jinsi wanavyofanya biashara yao na wanavyotozwa kodi katika Nchi nyingine”

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo alipoulizwa alisema

“Lengo ni kufikia mahali huko mbeleni ili kampuni hiyo ichangie kodi kwa pesa inayopata kutokana na biashara inayofanyika hapa nchini kupitia mitandao, Wananchi hawatakiwi kuwa na hofu yoyote kwasababu hii inahusu biashara inayofanyika na kampuni hiyo katika Nchi mbalimbali”

“Na hili sio jambo geni lipo dunia nzima, tumesikia Kenya tayari hilo lipo, Benin, Cameroon na Nchi za Ulaya ambako kampuni hizo kubwa za mitandao duniani zinachangia kodi kwa kufuata sheria za nchi husika na taratibu za kimataifa“- Kayombo

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
1 Comment

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive