Hatimaye, Twitter yakubali kununuliwa na Elon Musk kwa dola bilioni 44

Mwandishi Emmanuel Tadayo
Baada ya majuma kadhaa ya vuta nikuvute hatimaye, Twitter yakubali kununuliwa na Elon Musk kwa dola bilioni 44. Bodi yawakurugenzi ya mtandao wa kijamii wenye ushawishi mkubwa wa Twitter na Elon Musk wamefikia makubaliano kwamba kampuni hiyo itauzwa kwa karibu dola za marekani bilioni 44, Twitter imeandika katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumatatu. Wanahisa watalipwa dola 54.20 kwa kila hisa. Musk ni mmoja wa wanahisa wakubwa wa Twitter.

Muda mfupi baada ya habari hizo kuibuka, kampuni ya Twitter ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikithibitisha kuwa imekubali ombi la Musk la kuuchukua mtandao huo wa kijamii kuwa ataubinafsisha.

“Bodi ya Twitter ilifanya mchakato wa makini na wa kina ili kutathmini pendekezo la Elon kwa kuzingatia kwa makusudi thamani, uhakika, na ufadhili,” Mwenyekiti wa Bodi Huru ya Twitter Bret Taylor alisema juu ya mpango huo. “Shughuli iliyopendekezwa itatoa malipo makubwa ya pesa taslimu, na tunaamini ni njia bora zaidi kwa wamiliki wa hisa wa Twitter.”

 

Mwandishi Emmanuel Tadayo Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
mwandishi wa habari za teknolojia kwenye tovuti pendwa ya mtaawasaba
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive