Tukiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, tutajaribu kuangazia baadhi ya michango ya wanawake katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia . Orodha ni ndefu na mambo ni mengi ambayo wanawake wameweza kuishangaza dunia katika nyanja za sayansi na teknolojia. Kwa leo tutakuletea gunduzi saba ambazo zimeibadili dunia jumla.
1. Mashine ya kuoshea vyombo (Dish Washer)
Mwanamama Josephine Cochrane mnamo mwaka 1886 alifanikiwa kuvumbua mashine ya kwanza ya kuoshea vyombo ambayo iliweza kuuzwa madukani. Mashine hiyo ambayo ilitumia presha kubwa ya maji, kigurudumu, kifaa cha kuchemshia maji, na kichanja cha kuwekea vyombo vikisubiri kukauka baada ya kuoshwa. Hata hivyo mwanamama huyu hakuweza kuutumia ugunduzi wake japo alifanya maisha ya wafanyakazi wake kuwa rahisi.
2. Dawa ya fangasi (Nystatin)
3. Boya la kuokolea maisha (The life raft)
Boya hili liligunduliwa na mwanamama Maria Beasely mnamo mwaka 1882 baada ya siku moja kutazama baharini na kusema “watu hawatakiwi kufa kwenye chombo cha usafiri wa maji” kisha akabuni kifaa hicho ambacho kinaendelea kutumika mpaka leo japo kinafanyiwa maboresho ya hapa na pale.
4. Bomba la sindano
Bomba la sindano ni moja ya maajabu ya matibabu ya kisasa, mnamo mwaka 1899 mwanamama Letitia Geer alibuni bomba la sindano ambalo liliweza kushikwa mkono mmoja.
5. CCTV
Kutokana na tatizo la wizi lililokithiri na polisi kuwa wazito katika kabiliana na wezi katika jiji la New York, mnamo mwaka 1969 Mwanamama Marie Van Brittan Brown alibuni mfumo wa ulinzi kwa kutumia kamera ambao unamruhusu mtumiaji kuona kinachoendelea kupitia kwenye runinga akiwa ndani ya nyumba. Ugunduzi wake ndio mwanzo wa mifumo ya kisasa ya CCTV inayotumika majumbani na polisi mpaka sasa.
6. Programu ya kompyuta
Mnamo mwaka 1944 Dr. Grace Hopper alifanya ubunifu wa kompyuta katika chuo cha Havard iliyopewa jina la Mark I, kompyuta hii iliyokuwa na uzito wa tani tano na ukubwa wachumba kizima. Yeye ndio mwanzilishi wa neno “bug” akimaansha tatizo lililo kwenye programu ya kompyuta na neno “debugging” baada kuwa kuwatoa dudu washa waliokuwa wameingia ndani ya kompyuta hiyo.
Mama huyu programa wa kompyuta ndie mbunifu wa lugha ya kompyuta ya COBOL (kirefu chake ni COmmon Business-Oriented Language) ambayo mpaka leo hii bado inatumika.
Mjadala kuhusu wanawake waliofanya mambo makubwa katika nyanja za sayansi na teknolojia nchini na hata nje ya nchi unaweza kuendelea hapo chini kwenye box la maoni. Tupe maoni yako pia kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, facebook na Instagram kupitia akaunti yetu ya mtaawasaba.