VLC ni moja ya zawadi kubwa ya open-source. Ni moja kati ya media player ya kipekee ambayo iko stable, nyepesi kufunguka, isiyo na matangazo kabisa na inayocheza karibia kila aina ya mafaili ya muziki hata video na picha.
VideoLan kampuni iliyo nyuma ya VLC leo imachia toleo la 3.0 lililopewa jina la “Vetinari” la media player hii maarufu kwenye mifumo endeshi ya kompyuta na vifaa vya mkononi ikiwemo: Windows (ARM, x86, x64), macOS, Linux, Android, iOS, Android TV, Apple TV, bila kusahau Chrome OS. Ambapo toleo hili limetumia code moja kwa mifumo endeshi yote iliyotengenezwa. Unaweza ku download toleo hili jipya hapa: Android, iOS, na mifumo endeshi mingine hapa.
Kwa mujibu wa Jean-Baptiste Kempf, ambae ndio raisi wa VideoLan akiongea na mtandao wa VentureBeat amesema, toleo la 3.0 limekuja na vitu vingi vipya, kurekebisha makosa kama 1500 na marekebisho mengine zaidi ya 20,000. Na imechukua zaidi ya miaka mitatu ya kazi ya kujitolea kutoka kwa wachangiaji mbalimbali duniani kote tangu toleo la mwisho lilitoka Februari 2015.
Kabla hatujangaalia baadhi ya vitu vipya, inaweza kuwekwa kwenye mifumo endeshi ya zamani ikiwemo Windows XP na kuendelea, macOS 10.7 na kuendelea, Android 2.3 na kuendelea, Chromebooks ambazo zina Play Store, Apple TV, na Linux. Kwa mujibu wa bwana Jean-Baptiste Kempf, baadhi ya mifumo endeshi ndio litakuwa toleo la mwisho kuwekwa, VLC 4.0 haitaweza kuwekwa kwenye Windows XP na Vista, macOS 10.7 na 10.8, bila kusahau Android 2.x na 3.x.
Vitu vitano vikubwa vilivoongezwa kwenye VLC 3.0
- Uwezo wa ku Stream kwenye Chromecast
- Uwezo wa kucheza video za HDR na 10bit
- Uwezo wa kucheza video zilizo kwenye mfumo wa nyuzi 360 na sauti zilizo kwenye mfumo wa 3D
- Uwezo wa kucheza video za 4K na 8K bila kukwama
- Uwezo wa kupekua na kucheza mafaili yaliyo kwenye local network kama SMB, FTP, SFTP, NFS, na nyinginezo.
Sio hizi tu, kuna vipya lukuki vilivyo ongezwa kwenye toleo hili jipya la VLC 3.0. Ili uwezo kuona vitu vyote vilivyoongezwa, tembelea ukurasa maalumu uliowekwa kwa ajili ya toleo hili jipya hapa