Whatsapp yaacha kufanya kazi kwenye Windows phone na Blackberry

Alexander Nkwabi Maoni 162

Whatsapp imeacha rasmi ku support simu zenye mifumo endeshi ya kizamani ikiwemo BlackBerry OS, BlackBerry 10, na Windows Phone 8.

Kwenye ukurasa wao wa msaada kwa watumiaji wameandika:

Mifumo hii haina uwezo wa kumudu app hii kwa siku zijazo. Kama weweni mtumiaji wa moja ya mifumo itakayo athirika, tunashauri uhamie kwenye simu zenye mifumo ya kisasa zaidi, au toleo la Android kuanzia 4.0, iPhone yenye iOS 7+, au Windows Phone 8.1+ ili uendelee kupata WhatsApp

Once the dominant smartphone brand, BlackBerry was overtaken by Apple’s iPhone and Android devices, and today the brand is licensed to TCL, which makes Android devices under that name. And Microsoft, which once had big hopes for its smartphone business, has now largely exited that market.

Blackberry ambayo ilikuwa ni moja ya simu janja zenye jina kubwa ilipitwa na simu za iPhone na vifaa vya Android. Kwa sasa inaendeshwa na TCL ambayo inatengeneza Blackberry zinazotumia Android. Wakati kampuni ya Microsoft imeamua kuachana na utengenezaji wa simu janja.

Taarifa hizi sio za kushtua kwani tayari Whatsapp walishawapa taarifa watumiaji wa vifaa hivyo kuhusiana na kuacha kuvisapoti tangu mwezi wa pili 2016. Tayari WhatsApp hawasapoti vifaa vyenye mifumo endeshi ya zamani ikiwemo, matoleo ya Android kuanzia 2.3.3 kurudi nyuma, Windows Phone 7, iOS 6, na Nokia Symbian S60

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive