Apple kununua app ya kutambua muziki ya Shazam

Mwandishi Alexander Nkwabi

Taarifa ambazo zimeanza kuonekana Tech Crunch zinasema kuwa Kampuni ya Apple iko katika hatua za mwisho kabisa kukamilisha dili la kuinunua app ya Shazam, programu inayokuwezesha kutambua nyimbo, matangazo au hata vipindi vya runinga kwa kuisikilizisha tu na inakuletea majibu ndani ya sekunde chache.

Kwa mujibu wa taarifa iyo, dili hilo la kuinunua Shazam lilisainiwa wiki hii, na inasemekana litatangazwa rasmi jumatatu (japo mambo yabnaweza kubadilika).

Chanzo kimoja cha habari kinadai dili hilo ni la tarakimu tisa na chanzo kingine kinadai ni dola za kimarekani 401, haijawekwa wazi bado.

Shazam imekuwepo tangu mnamo mwaka 1999, ambapo jina lake la mwanzo lilikuwa 2580, ambayo ilikuwa ni namba unayopiga kwenye simu yako kuipata huduma hiyo huko Uingereza.

Ukiachana na dili hili, Apple imeshafanya manunuzi mengi na moja kati ya manunuzi makubwa kabisa ni katika eneo la muziki, ambapo mwaka 2014 Apple ilinunua Beats kwa dola za kimarekani bilioni 3, na kuifanya kama msingi wa Apple Music, huduma ambayo kwa sasa ina watumiaji milioni 30.

Tutaendelea kukujuza zaidi kuhusiana na habari hii

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive