Facebook yathibitisha kufanya majaribio ya kitufe cha downvote

Mwandishi Alexander Nkwabi

Kwa miaka sasa, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook wakiomba kuongezwe kitufe cha “Dislike” lakini haikuwahi kutokea ivyo. Badala yake kumekuwa na kitufe kingine kimeanza kuonekana kwa baadhi ya watu.

Siku ya alhamisi, watu kadhaa wameanza kuona kitufe cha Downvote kwenye sehemu ya comment ndani ya magrupu ya Facebook na kwenye kumbukumbu za zamani. Watumiaji kadhaa wamekuwa wakisambaza screenshot za kitufe icho.

kitufe cha downvote

Hata hivyo msemaji wa Facebook amekanusha kufanya majaribio ya kitufe cha Dislike. Amesema “Hatufanyii majaribio kitufe cha dislike. Tunajaribu kitu kipya ambacho watu watatupa mrejesho kwenye maoni kuhusiana na post kwenye makundi ya Facebook. Kwa sasa tunafanya majaribio kwa kundi dogo la watu kwa Marekani pekee.”

Majaribio yanafanyika kwa 5% ya watumiaji wa Marekani ambao wameweka lugha ya Kiingereza. Kitufe kitatokea kwenye machapisho yaliyo post zinazoonekana na watu wote na sio kwenye vikundi, watu maarufu au watumiaji wa kawaida. Kwa sasa hawana mpango wa kuongeza watu zaidi kwa ajili ya majaribio.

Lengo la kitufe hicho cha Downvote kinapoguswa ni kushusha comment ambayo inaonekana “inakarahisha”, “inapotosha” au “nje ya mada”. Ni moja ya jitihada za Facebook kuhakikisha taarifa halisi kwa watumiaji na kuondoa vitu visivyo na maana kwenye taarifa wanazosoma.

Kitufe hiki kitasababisha “kuzika” maoni na watu wanazichapisha. Hata hivyo hili linaweza kuleta maswali mengi kuhusu uzuiaji wa taarifa (censorship) na maoni yapi yanatakiwa yawe “yanakarahisha”, “yanapotosha” au “yako nje ya mada”.

Muanzilishi wa mtandao wa kijamii wa  Reddit, Bwana Alexi Ohanian ameandika kwenye twitter yake kuvutiwa na hatua ya Facebook kuweka kitufe hicho, kitufe kama hicho kimekuwepo kwenye mitandao mingi ya kijamii ikiwemo Reddit ambayo imekipa umaarufu.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Mtaawasaba, usisahau kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram, pia usisahau ku subscribe kama bado hujafanya hivyo  ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka kila zinapotoka tu.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive