Meta/Facebook yashika namba 1 kampuni mbaya Zaidi mwaka 2021

Mwandishi kasomi

Kila mwaka Yahoo Finance inatoa ripoti za kampuni za mwaka. Watu wanapata nafasi ya kupiga kura.

Kampuni ya Facebook/Meta imechukua nafasi ya “The Worst Company of the Year”. Facebook imeongoza kwa kupata kura nyingi na asilimia kubwa ya walioshiriki kutoa maoni wanaona muelekeo wa Facebook umepotea.

Sababu kubwa ni kuhusu data za whistleblowers ambao walikuwa wafanyakazi wa Facebook waliotoa siri na ripoti kuhusu madhara ya FB kwa watoto na madhaifu ya algorithm yake. FB imeonekana ilishindwa kupambana na habari za uongo, vikundi vya fujo na algorithm yake inafocus na addiction kuliko afya ya akili kwa watumiaji wake.

Facebook mwaka huu imeanza kusafisha jina lake kwa kubadili jina la kampuni kuu kuwa Meta na kufuta mfumo wa Facial Recognition. FB inaelewa taswira yake ambayo imezidi kupotea. Hasa katika kipindi ambacho kuna competition katika platforms nyingine kama TikTok, YouTube, Snapchat, Twitter, Reddit, n.k.

Ni kweli FB inastahili kuwa kampuni mbaya ya mwaka?

Mwandishi kasomi Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Mwandishi | mhamasishaji | mwanafalsafa | blogger | Host | Personalty TV & Radio presenter @Kasomi TV
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive