Meta imetengeneza Haptic Gloves zenye hisia na uwezo wa kugusa vitu katika ulimwengu wa kidigitali

Mwandishi kasomi

Kabla ya Facebook kujiita Meta, imewekeza kwa ukubwa katika majaribio ya vifaa vya VR na kuanzisha Meta Reality Labs ambayo inafanya utafiti na kutengeneza viungo bandia, vifaa vya VR vya kuvaa, mifumo ya AR/VR na teknolojia ya kutafsiri hisia za mwili na kuunganisha na vifaa vya kiteknolojia.

Wiki hii, Meta imeonyesha Gloves mpya zenye uwezo wa kuweka uhalisia wa miguso katika ulimwengu wa kufikirika. Gloves hizi zimefungwa teknolojia maalum ambazo zinawezesha mtu ku-kuhisi miguso, vitu na kuweka uhalisi wa kushika vitu na miguso katika ulimwengu wa kidigitali.

Gloves hizo, zina uwezo wa kushirikiana na VR na mtu akapata uhalisia wa kuona na kugusa vitu, Mfano mtu anaweza kujenga, kushika vitu katika ulimwengu wa kidigitali na kuhisi kama ni uhalisia.

Mwandishi kasomi Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Mwandishi | mhamasishaji | mwanafalsafa | blogger | Host | Personalty TV & Radio presenter @Kasomi TV
1 Comment
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive