Donald Trump azindua rasmi Mtandao wa Truth Social

Mwandishi kasomi
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump azindua rasmi Mtandao wa kijamii wa Truth Social. Mtandao huo ulizinduliwa jana Februari 16, 2022.

Uamuzi wa kuanzisha Mtandao wa Truth Social ulikuja baada ya mitandao ya Facebook na Twitter kumfungia kutumia mitandao hiyo kutokana na kuhusika na kuhamasisha shambulio katika jengo la Capitol Januari 6, mwaka 2021

Kupitia taarifa kwa waandishi wa habari, Trump Media & Technology Group (TMTG) ambayo ndio inasimamia mtandao huo wa kijamii wa Mtandao wa Truth Social imesema kwamba mkakati wao ni kuwapa watu uwezo wa kuongea kutokana na mitandao yenye mirengo ya kiliberari kuwa na nguvu ya kunyamazisha sauti za wamarekani.

Mpaka sasa Mtandao wa Truth Social unaendelea kufanya vyema kwani umepakuliwa zaidi ya mara elfu 50 (kipindi habari hii inaandikwa) kupitia appstore na Google Play Store

Haya ni machache unatakiwa kufahamu kuhusu Mtandao wa Truth Social;

  • utaanza kupatikana rasmi kwa watumiaji wote kuanzia tarehe 21, februari 2022
  • Mtandao wa Truth Social utakuwa bure kudownload
  • haijajulikana kama utakuwa ni watumiaji wote dunia nzima au marekani tu
  • kutakuwa na huduma zitakazo hutaji kulipiwa ili uzipate.

Kwa habari motomoto zaidi kuhusu teknolojia, endelea kutembelea tovuti yetu bila kusahau kuacha maoni yako kuhusu makala husika, Pia usisahau kutufollow kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, facebook, Instagram na youtube.

Mwandishi kasomi Mchangiaji
Mitandao ya Kijamii
Mwandishi | mhamasishaji | mwanafalsafa | blogger | Host | Personalty TV & Radio presenter @Kasomi TV
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive