Nokia 6 (2018) yatangazwa

Mwandishi Alexander Nkwabi

Jana kulivuja taarifa kwenye mitandao kuhusu simu ya Nokia 6 (2018). Basi leo kupitia tovuti yao, Nokia wametangaza rasmi kutoka kwa Nokia 6 (2018).Mtaawasaba nokia 6 2018 18

Jina halisi la simu hii ni Nokia 6 (second generation) na inaonesha itakuwa na karibu sifa nyingi za mtangulizi wake aliyetoka mwaka jana Nokia 6 (2017). Simu hii inakuja na mfumo endeshi Android Nougat ambapo inaweza kupandishwa hadhi mpaka Android Oreo.

  Mtaawasaba nokia 6 2018 17
Simu hii inakuja na chip ya Qualcomm Snapdragon 630 (mtangulizi wake alikuja na Snapdragon 430) pia inakuja na teknolojia ya kurekodi sauti ya OZO, na itakuwa na Bothie photo mode kwenye upande wa kamera.
Mtaawasaba nokia 6 2018 16
Unaweza kuoda simu yako mapema hata kabla haijatoka kuanzia leo, ambapo simu yenye ukubwa 32GB itauzwa kwa dola za kimarekani 230 wakati yenye 64GB itaenda kwa dola za kimarekani 245, na simu itaanza kupatikana kuanzia mwezi wa kwanza mnamo tarehe 10. Tutegemee kuiona simu hii kwenye maonesho ya CES 2018 yanayoanza wiki ijayo.Mtaawasaba nokia 6 2018 20

Uchambuzi wa simu hii utaupata kwenye kipengele cha uchambuzi

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive