Ripoti: Tanzania yafikisha watumiaji wa Intaneti milioni 23

Mwandishi Alexander Nkwabi

Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika ripoti za robo ya nne ya mwaka inayoishia Desemba 2017 inaonesha ongezeko kubwa la watumiaji wa huduma ya Intaneti kufikia asilimia 45 ya watanzania ambayo ni sawa na watu milioni 23 ukilinganisha na watanzania milioni 7.52 ambao ni sawa na asilimia 12 tu ya watanzania mwaka 2012.

3

Ongezeko la watumiaji linaonesha kwa mwaka 2013 kulikuwa na watumiaji milioni 9.31 sawa na asilimia 21 ya watanzania wote, idadi ya watumiaji iliendelea kupanda kufikia watanzania milioni 12.27 sawa na asilimia 29 ya watanzania wote kwa mwaka 2014. Idadi imezidi kuongezeka mwaka hadi mwaka kama inavoonekana kwenye kielelezo hapo chini.

#ffffff;">
MwakaIdadi ya watumiajiAsilimia (ya watanzania)
2012milioni 7.5212
2013milioni 9.3121
2014milioni 12.2729
2015milioni 17.6234
2016milioni 19.8640
2017milioni 2345

 

Katika ripoti ya mwaka 2018 ya Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) yenye jina “Achieving universal and affordable internet in the least developed countries’ iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Januari inaeleza kuwa jitihada za kuboresha sera zinazohusu Tehama na uwekezaji katika mkongo wa Taifa wa mawasiliano (NICTBB) ni baadhi ya mambo yaliyofanya Tanzania ifanikiwe kuchochea ukuaji wa matumizi ya intaneti. Ambapo Tanzania ilikopa Dola za Marekani milioni 170 (zaidi ya Sh377 bilioni) kwa awamu mbili kutoka benki ya Exim ya China ili kugharamia mkongo huo wa taifa wa mawasiliano uliosambaa nchi nzima.

Kasi ya ukuaji wa intaneti ni moja ya hatua muhimu ya Tanzania katika kufikia malengo ya ukuaji wa uchumi

Kasi ya ukuaji wa intaneti ni moja ya hatua muhimu ya Tanzania katika kufikia malengo ya ukuaji wa uchumi kwa kutumia Tehama ifikapo mwaka 2020 kama ilivyobainishwa katika lengo namba 9.c la Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

2

Pia katika ripoti hii iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  inaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imeongezeka na kufikia watumiaji milioni 40 kutoka watumiaji milioni 27.62 kwa mwaka 2012,  mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania ukiongoza kwa kuwa na watumiaji waliojisajiliwa 12,714,297 wakifuatiwa na Tigo kwa kuwa na watumiaji waliosajiliwa 11,062,852.

2.5

Katika taarifa hiyo inaonesha aina ya intaneti inayotumika kama simu za mkononi, watumiaji wa intaneti inayohamishika ni takribani watu 19,006,223 huku watumiaji takribani milioni 3.47 wanatumia intaneti ya ‘wireless’ isiyohamishika na watumiaji wapatao 520,698 wanatumia ‘wired internet’ isiyohamishika .

2.3Unaonaje kuhusu takwimu hizi na ongezeka hili la watumiaji wa intaneti Tanzania? Tuandikie maoni yako kwenye sehemu ya kuacha maoni. Pia usisite kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kama Fecebook, instagram na Twitter.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive