Imethibitishwa huduma hii mpya ya View Once itaanza kutumika wiki hii.
WhatsApp wamedai kuwa hii ni njia salama kutuma na kupokea taarifa nyeti bila kuhifadhiwa au kuonwa zaidi ya mara moja kwani watumiaji watakaokuwa hewani pekee ndio wataweza kuona video na picha za namna kabla hazijafutika
Tayari mitandao kadhaa ya kijamii kama Snapchat, Telegram na Instagram imekuwa na huduma kama hii ambayo huwaruhusu watumiaji kutuma jumbe zinazojifuta mara baada ya kufunguliwa.
Kutoka kwenye blogu ya mtandao huu wa kijamii unaomilikiwa na kampuni ya Facebook iliandikwa,
“ kupiga picha na video imekuwa ni sehemu ya Maisha yrtu, japo si kila tunachoshea lazima kibaki kwenye rekodi za kidijitali moja kwa moja,
Ndio maana leo tunaachia hiki kipengele kipya cha kuona mara moja picha na video ambazo zitatoweka mara baada ya kuziona mara moja, hii itawapa watumiaji uwezo Zaidi wa kusimamia faragha zao”
Mara tu picha au video itakapofunguliwa na kisha ki=utoweka, mahala palipokuwepo picha/video hiyo pataandikwa “opened” ili kuondoa mkanganyiko, wameandika WhatsApp.
Hata hivyo kwa maandishi madogo sana wameandika “kipengele hiki hakita zuia wat uku screenshot picha kabla haijafutika”.
Una maoni gani kuhusu huduma hii mpya iloachiwa na WhatsApp? Andika maoni yako hapo chini.