YouTube imeamua kuficha idadi ya dislikes kwenye video zote

Mwandishi Alexander Nkwabi
Kuanzia leo, YouTube imeamua kuficha idadi ya dislikes kwenye video zote zilizopo katika mtandao huo mkubwa wa video unaomilikiwa na Google.

 Mabadiliko haya yanaweza kubadili kwa kiasi kikubwa namna tabia za watumiaji wa mtandao huo. Hata hivyo taarifa hii inasema, kinachoondolowa ni idadi ya dislike na sio kitufe cha dislike. Idadi ya ambao hawakuipenda video itaonekana na aliyechapisha video iyo pekee. Kuanzia sasa watumiaji wataweza ku dislike video ila hawataweza kuona idadi ya dislike kwenye video hiyo.

Sababu kubwa iliyowafanya YouTube kuficha idadi ya dislikes kwenye video zote ni kuwalinda watengenza maudhui wadogo, wanaochipukia dhidi ya mashambulio ya makusudi ya dislikes na kukerwa kwa makusudi, Pia YouTube wamesema wanataka kusisitiza kwenye muingiliano wenye heshima kati ya watazamaji na watengeneza maudhui. Kama tulivoandika huko juu, mabadiliko haya hayata waathiri watengeneza maudhui ila yatawaathiri watazamaji, ambapo watengeneza maudhui wataendelea kuona idadi ya ambao hawakuipenda video husika kupitia YouTube Studio.

Mabadiliko haya yaliyofanya mpaka YouTube imeamua kuficha idadi ya dislikes kwenye video zote hayajaja tu kutoka hewani, mwezi wa machi YouTube walitangaza watafanya utafiti wa kuondoa idadi ya dislike kwa kikundi cha watumiaji wachache. Na majibu ya utafiti huo yakaonesha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa tabia ya kushambulia kwa makusudi. Pia utafiti huo ukagundua, dislike za makusudi zinatokea kwa wingi kwenye channel au watengeneza maudhui wadogo au ambao wanachipukia.

Chapisho kwenye blog ya YouTube limeandika,  

“We heard during the experiment that some of you have used the public dislike count to help decide whether or not to watch a video. We know that you might not agree with this decision, but we believe that this is the right thing to do for the platform,” 

Kwa mujibu wa Wikipedia, YouTube kupitia video yake ya YouTube Rewind 2018 ndio imekuwa ikishika rekodi ya kuwa na uwiano mkubwa wa dislike na like kwenye mtandao huo ambapo mpaka sasa tunapoandika chapisho hili ina dislike milioni 19.67 (na like milioni 3 tu) ikiipiku video ya Justin Bieber – Baby iliyokuwa ikishika rekodi iyo. Inasemekana ni moja ya sababu ya YouTube kuacha utamaduni wa kuachia video za YouTube Rewind ambazo hutoka mwishoni mwa mwaka zikiangazia mambo mbalimbali yaliyojiri kwa mwaka husika.

Japokuwa maamuzi haya yatawasaidia watengeneza maudhui, kwa watazamaji italeta changamoto kidogo, kwanza itakuwa ngumu kwa mtazamaji kuchagua video maana moja ya vigezo vya watazamaji uwa ni uwiano wa like na dislike wakati wa kuchaua video ya kuangalia. Pia matapeli wataweza kutumia fursa hii kutoa video zitakazojifanya kama ndio halisi.

Mabadiliko haya unayoanaje? tuandikie kwenye upande wa comment, pia kupitia mitandao ya twitter, instagram na facebook.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive